Sheria za Huduma

Bull City Learning, Inc.

Sheria za Huduma

Ilisasishwa mwisho: Machi 23, 2020

Sheria hizi za huduma zinajumuisha makubaliano ya kisheria baina yako, iwe kibinafsi au kwa niaa ya shirika fulani ("wewe", "mtumiaji", au "yako/zako") na Bull City Learning, Inc., ikijumuisha washirika ("Bull City Learning", "sisi", "yetu", au "zetu"), kuhusiana na ufikiaji wako na matumizi yako ya tovuti zetu, na pia aina nyingine yoyote ya midia, mfumo wa midia, tovuti ya rununu au programu ya rununu inayohusiana au vinginevyo iliyounganishwa nazo (kwa pamoja, "Tovuti"). Unakubali kwamba kwa kufikia Tovuti, umesoma, kuelewa, na kukukubali kuambatana na Sheria hizi zote za Huduma. UKIKOSA KUKUBALIANA NA SHERIA HIZI ZA HUDUMA, BASI UNAPIGWA MARUFUKU KABISA YA KUTUMIA TOVUTI NA NI LAZIMA UACHE KUITUMIA MARAMOJA.

Sheria na masharti ya ziada au hati za ziada ambazo mara kwa mara huenda zikachapishwe kwenye Tovuti zinajumuishwa hapa kwa marejeleo. Kwa hiari yetu pekee, tunahifadhi haki ya kufanya mabadiliko au marekebisho kwenye Sheria hizi za Huduma wakati wowote kwa sababu yoyote. Tutakuarifu kuhusu mabadiliko yoyote kwa kusasisha tarehe ya "Ilisasishwo mwisho" ya Sheria hizi za Huduma, na unaondoa haki yoyote ya kupokea ilani maalum ya kila badiliko linalofanywa. Ni jukumu lako kupitia Sheria hizi za Huduma mara kwa mara ili kupata ufahamu kuhusu masasisho. Ukiendelea kutumia Tovuti baada ya tarehe mnamo Sheria za Huduma zilizosasishwa zinapochapishwa, itachukuliwa kwamba umefahamishwa na ukakubali mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria zozote za Huduma zilizosasishwa.

Maelezo yaliyotolewa kwenye Tovuti hii hayakusudiwi kusambazwa wala kutumiwa na mtu au mhusika yeyote katika mamlaka au nchi yoyote ambapo usambazaji huo au matumizi hayo yatakuwa kinyume cha sheria au kanuni au ambako tutahitajika kujisajili ndani ya mamlaka au nchi hiyo. Ipasavyo, watu wanaochagua kufikia Tovuti wakiwa katika maeneo mengine wanafanya hivyo kwa uamuzi wao binafsi na wanawajibika peke yao katika kuambatana na sheria za eneo husika, ikiwa sheria za eneo hilo zinahusika na kwa kiwango ambacho zinahusika.

Tovuti inakusudiwa watumiaji ambao wana umri wa angalau miaka 18. Watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kutumia wala kujisajili kutumia Tovuti.


SERA YA USIRI

Bull City Learning inaheshimu usiri wa watumiaji wa Huduma zake.  Tafadhali rejelea Sera ya Usiri ya Bull City Learning ambayo inaelezea jinsi ya tunavyokusanya, tunavyokutumia, na tunavyofichua maelezo yanayohusiana na usiri wako.  Kwa kutumia Tovuti hii, unakubali kuambatana na Sera yetu ya Usiri, ambayo imejumuishwa katika Sheria hizi za Huduma. Tafadhali fahamu kwamba Tovuti inapeperushwa mtandaoni kutoka Marekani. Ukifikia Tovuti kutoka Umoja wa Ulaya, Asia, au eneo nyingine lolote ulimwenguni ambalo lina sheria au kanuni nyingine zinazotawala ukusanyaji, matumizi, au ufichuaji data za kibinafsi ambazo zinatofautiana na sheria za Marekani, basi kuendelea kutumia Tovuti, unahamisha data zako hadi Marekani, na unatoa idhini ya data zako kuhamishwa hadi na kusindikwa nchini Marekani.

Aidha, kwa ufahamu hatukubali, kuomba, wala kudai maelezo kutoka kwa watoto wala kufanya uuzaji kwa watoto. Hivyo basi, kulingana na Sheria ya Marekani ya Ulindaji Usiri wa Watoto Mtandaoni (kama ilivyorekebishwa), tukipokea maelezo ya kweli kwamba mtu yeyote wa chini ya umri wa miaka 13 ametupatia maelezo ya kibinafsi bila idhini hitajika na inayoweza kuthibitishwa kutoka kwa mzazi, basi tutafuta maelezo hayo kutoka kwenye Tovuti haraka iwezekanavyo.


KUHUSU HUDUMA

Maudhui, programu, bidhaa, na/au huduma zinaotolewa kwenye Tovuti ("Huduma") zimebuniwa kukuwezesha kufikia maelezo fulani kwa maandishi, video, au mengine yanayohusiana na mada za chanjo, afya ya akina mama, na huduma msingi ya afya.  

USAJILI; MASHARTI YA TABIA YA MTUMIAJI; MATUMIZI YA HUDUMA

Huenda ukahitajika kujisajili kwenye Tovuti. Unakubali kuweka nenosiri lako kwa usiri na utawajibikia matumizi yote ya akaunti yako na nenosiri lako. Tunahifadhi haki ya kuondoa, kukupokonya, au kubadilisha jina la mtumiaji unalochagua tukibainisha, kwa hiari yetu pekee, kwamba jina hilo la mtumiaji si mwafaka, ni chafu, au vinginevyo halikubaliki. Unakubali kutuarifu maramoja kuhusu matumizi yoyote ya nenosiri lako na/au akaunti yako bila idhini. Bull City Learning haitawajibikia hasara zozote zinaoibuka kutokana au kuhusiana na matumizi ya jina lako la mwanachama, nenosiri lako, na/au akaunti yako bila idhini.


[WIGO WA HUDUMA]

 • BCLi  (Bull City Learning Institute)

  Tovuti ya kimaelezo ya BCL Institute for Learning in Global Health, mtoaji suluhu ya mafunzo kwa mada za chanjo, afya ya akina mama, na huduma msingi ya afya. Kwenye ukurasa huu wa tovuti, watumiaji wanaweza kufikia suluhu mbalimbali za mafunzo ikijumuisha kozi ya bidhaa za  Immunization Academy : IA Watch, IA Learn, IA Score, na IA Manage. 

 • Immunization Academy's IA Watch 

  Jukwaa la video lililo na zaidi ya video fupi 100 za mafunoz ya chanjo kwa lugha za Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa. Watumiaji wanaweza kupata alama kwa mafanikio ya mafunzo, kutengeneza orodha ya uchezaji, na kupakua video ili kutazamwa nje ya Intaneti. Kwa urahisi watumiaji wanaweza kufikia video nje ya Intaneti na kwenye vifaa vyao tamba kupitia programu ya Android ya IA Watch. Watumiaji waliosajiliwa wanaweza kutazama shughuli na mafanikio ya watumiaji wengine waliosajiliwa ikijumuisha video zilizotazamwa, video zilizopendwa, na beji walizopata.

 • Immunization Academy's IA Learn 

  Jukwaa la bila malipo la Mafunzo ya Mtandaoni kwa wataalamu wa chanjo, linalowawezesha kukamilisha kozi kuhusu mada kama vile “cold chain”, ufuatiliaji, na uwasilishaji chanjo.  

 • Immunization Academy's IA Score 

  Zana ya tathmini kwa wataalamu wa chanjo, inayowawezesha kutambua pengo za ujuzi na maarifa kwenye ngazi ya kiwilaya, kieneo, au kitaifa. 

 • Immunization Academy's IA Manage 

  Dashibodi ya uchambuzi wa mafunzo kwa mameneja wa chanjo, inayowawezesha kufuatilia utendakazi wa watu binafsi na timu, kupeana kozi, na kupata maelezo kuhusu ripoti za data za mafunzo. 


MASHARTI YA MALIPO

Huenda ukahitajika kununua au kulipa ada ili kufikia Maudhui yetu. Unakubali kutoa maelezo ya sasa, kamili, na sahihi ya ununuzi na akaunti kwa manunuzi yote unayofanya kupitia Tovuti. Pia unakubali kusasisha maelezo ya akaunti na malipo bila kuchelewa, ikijumuisha anwani ya barua pepe, mbinu ya malipo, na tarehe ya mwisho ya kadi ya malipo, ili tuweze kukamilisha miamala yako na kuwasiliana nawe inavyohitajika. Tutakutoza bili kupitia akaunti ya bili ya mtandaoni kwa manunuzi unayofanya kupitia Tovuti. Ushuru wa mauzo utaongezwa kwenye bei ya manunuzi kama inavyohitajika nasi. Huenda tukabadilisha bei wakati wowote. Malipo yote yatafanywa kwa dola za Marekani kupitia (i) kadi halali ya mkopo inayokubalika na Bull City Learning, au (ii) mbinu nyingine yoyote ya malipo inayokubalika na Bull City Learning.

Unakubali kulipa ada zote kwa bei za wakati huo unapofanya manunuzi, na unatuidhinisha kutoza mto huduma ya malipo yako kwa viwango hivyo baada ya kufanya ununuzi wako. Ikiwa ununuzi wako ni wa kutozwa ada za kujirudia rudia, basi unatoa ridhaa ya sisi kutoza mbinu yako ya malipo mara kwa mara bila kuhitajika kuomba idhini yako kwanza ili kutoza ada hizo, mpaka utuarifu unataka kusitisha ada hizo. Aidha, unaelewa na kukubali kwamba tunatoa bili na kutoza ada kwa ajili ya Maudhui unayonunua kutoka kwetu kwenye Tovuti, na kwamba sisi hatuhusiki katika makubaliano yoyote baina yako na mtumiaji mwingine yeyote kwenye Tovuti wala hatuwajibikii majukumu ulionayo kwa mtumiaji huyo mwingine.

Tunahifadhi haki ya kusahihisha hitilafu zozote katika bei, hata kama tayari tumeshaagiza au kupokea malipo. Pia tunahifadhi haki ya kukataa ununuzi wowote uliofanywa kupitia Tovuti.

USITISHAJI, MIGOGORO, NA UREJESHAJI FEDHA

Fedha za manunuzi yaliyofanywa haziwezi kurejeshwa isipokuwa Bull City Learning iamue kurejesha fedha hizo, jambo ambalo litaamuliwa na Bull City Learning kwa hiari yake pekee kulingana na kila tukio. Hauna haki ya kurejeshewa fedha zozote kwa manunuzi yaliyofanywa kwenye Tovuti au kupitia Huduma. Unaweza kusitisha usajili wako wakati wowote kwa kuwasiliana nasi ukitumia anwani ya KUWASILIANA NASI iliyotolewa hapa chini. Unakubaliana na juhudi zetu za kibiashara za kushirikiana nasi kuhusiana na migogoro yoyote inayohusu manunuzi yaliyofanywa kwenye Tovuti. Usitishaji wako utaanzia mwishoni mwa muhula wa sasa wa malipo.

VIKWAZO VYA MATUMIZI

Kwa kutumia Tovuti, unawakilisha na kutoa hakikisho kwamba: (1) maelezo yote ya usajili unayowasilisha yatakuwa ya kweli, sahihi, ya sasa, na kamili; (2) utadumisha usahihi wa maelezo hayo na utasasisha maelezo hayo ya usajili inavyohitajika bila kuchelewa; (3) una uwezo wa kisheria na unakubali kuambatana na Sheria hizi za Huduma; (4) wewe si mtoto katika mamlaka unakoishi; (5) hautafikia Tovui kupitia njia zisizo za kibinadamu, iwe ni kwa kutumia roboti ya kompyuta, programu au vinginevyo; (6) hautatumia Tovuti kwa madhumuni yoyote haramu au ambao hayajaidhinishwa; (7) matumizi yako ya Tovuti hayatakiuka sheria au kanuni husika; na (8) una leseni na vyeti sahihi, halali na zilivyosasishwa ambazo kwenye Tovuti umetaja kuwa unamiliki (ikiwa umetaja).

Ukitoa maelezo yoyote ambayo si ya kweli, si sahihi, si ya sasa, au si kamili, tuna haki ya kuahirisha au kufunga akaunti yako na kukukataza matumizi yoyote na yote ya sasa au ya siku zijazo ya Tovuti (au sehemu yake yoyote).

Bila kujali yaliyotajwa hapo awali, ikiwa wewe ni (au unawakilisha, au unadai kuwakilisha) mhusika yeyote, kwa kutumia Tovuti na/au Huduma unawakilisha na kutoa hakikisho kwamba utekelezaji, uwasilishaji na utendakazi chini ya Sheria hizi za Huduma, na ukamilishaji wa miamala iliyotolewa hapa chini, yameidhinishwa kikamilifu na mhusika na kwamba mtu/watu wanaotumia Tovuti na/au Huduma kwa niaba yake wana uwezo kamili wa kumhusisha mhusika.

Ruhusa yako ya kutumia Huduma inategemea vikwazo vifuatavyo vya matumizi na tabia. Haswa, unakubali kwamba kwa hali zozote hautafanya yafuatayo:

 • kutuma maelezo yoyote ambayo ni ya matusi, kutisha, machafu, kuharibiana jina, ya upinzani, au hayakubaliki na ni mabaya kimbari, kijinsia, kidini, au vinginevyo hayakubaliki na ni ya kudhuru;
 • kutumia Huduma kwa madhumuni yoyote yaliyo ya kisheria au kuunga mkono shughuli haramu;
 • kunyanyasa, kumtumia vibaya au kumdhuru mtu mwingine au kundi nyingine au kujaribu kufanya hayo;
 • kutumia akaunti ya mtumiaji mwingine bila ruhusa;
 • kutoa maelezo ya uwongo au yasiyo sahihi unaposajili akaunti;
 • kuhitilafiana na utendakazi mwafaka wa Huduma au kujaribu kufanya hilo;
 • kutumia mfumo kwa njia otomatiki, au kuchukua hatua tunayoichukulia kuwa inasababisha mzigo mzito kwenye seva zetu au msingi wa mtandao wetu;
 • kuepuka vichwa vya kutenga roboti au hatua nyingine tunazochukua ili kuzuia ufikiaji Huduma au kutumia programu, teknolojia, au kifaa ili kudukua Huduma au kuchuma au kubadilisha data; au kuchapisha au kuunganisha na maudhui haribifu yanayokusudiwa kuharibu au kuhitilafiana na kivinjari au kompyuta ya mtumiaji mwingine.

MAELEZO YANAYOTUMIKA BAINA YA WATUMIAJI; UTUMAJI UJUMBE BAINA YA WATUMIAJI

Matumizi yako ya Tovuti yanaweza kuhusu kusajili akaunti kwenye Tovuti na kutengeneza wasifu wa kibinafsi kwa ambao unaweza kupakia maelezo fulani ya kibinafsi, ikijumuisha picha yako ya wasifu, jina, eneo (nchi), cheo cha kitaalamu, lugha inayopendelewa, na shughuli za akaunti (video ulizotazama, video ulizohifadhi kwenye orodha za utazamaji, video "ulizopenda", beji ulizopata, na video ulizoshiriki za wengine. Kimsingi, maelezo haya yanapatikana kuonwa na watumiaji wengine waliosajiliwa. Hata hivyo, una chaguo la kufanya baadhi ya maelezo haya kuwa ya siri/kibinafsi na hivyo basi hayataonwa na watumiaji wengine waliosajiliwa. Bado utaweza kutazama maelezo ya watumiaji wengine ambayo yanaweza kuonekana. Maelezo ya wasifu yanaweza kuonwa tu na watumiaji wengine ambao wameunda akaunti iliyosajiliwa; hayawezi kuonwa na watu wanaotembelea tovuti bila kusajili akaunti.

Matumizi yako ya Tovuti huenda yakahusisha Huduma zinazowezesha mawasiliano baina yako na watumiaji wengine kupitia jukwaa la ujumbe wa majadiliano au mbinu za mawasiliano za kielektroniki. Idadi ya ujumbe unaopokea, na kana kwamba unapokea ujumbe wowote au la, inatofautiana kulingana na Huduma unazotumia na kiwango cha utangamano wako na watumiaji wengine wa Tovuti.

Mawasiliano yote baina yako na watumiaji wengine yako chini ya Vikwazo vya Matumizi vilivyo hapa juu na Kanusho la Maudhui Mtandaoni lililo hapa chini. Unakubali kutuondolea lawama kikamilifu kwa madai, gharama, na hasara zote zinazoibuka kutokana au kuhusiana na ukosefu wako wa kuambatana na sheria hizi. Ukiamua kushiriki maelezo ya kibinafsi na watumiaji wengine kupitia mawasiliano baina yako na wao kwenye Tovuti, unafanya hivyo kwa shauri yako, kwani hatuwezi kutoa hakikisho kwamba usiri wa maelezo hayo ya kibinafsi utalindwa. Aidha, ikiwa mawasiliano baina yako na watumiaji wengine kwenye Tovuti yatapelekea, mbinu nyingine za mawasiliano za nje ambazo hazihusiani na Tovuti, unawakilisha na kukiri kwamba mawasiliano hayo hayako chini ya ulinzi wa Sheria hizi za Huduma wala Sera yetu ya Usiri. Unajihusisha katika mawasiliano hayo kwa shauri yako.

KANUSHO LA MAUDHUI MTANDAONI

Maoni, nukuu, ushauri, makadirio, kauli, ofa, au maelezo au maudhui mengine yanayopatikana kupitia Tovuti, lakini sio hayatolewi moja kwa moja na Bull City Learning ("Maudhui ya Mtumiaji"), ni ya waandishi husika, na si ya kutegemewa.  Waandishi hao wanawajibikia maudhui hayo wenyewe binafsi.  Bull City Learning haitoi hakikisho la usahihi, ukamilifu, au umuhimu wa maelezo yoyote kwenye Tovuti na Bull City Learning haitumii wala kuunga mkono, wala Bull City Learning haiwajibikii, usahihi au uaminifu wa Maudhui yoyote ya Mtumiaji.  Bull City Learning haiwajibikii wala kuchukua dhima kwa Maudhui yoyote ya Mtumiaji ambayo wewe au mtumiaji mwingine yeyote au mhusika mwingine anayochapisha au kutuma kupitia Huduma.  Hakuna wakati ambapo Bull City Learning itawajibikia hasara zozote zinazotokana na mtu yeyote kutegemea maelezo au maudhui mengine yaliyochapishwa kwenye Tovuti, au kutumwa kwa watumiaji.

Ingawa Bull City Learning inajitahidi kutekeleza Sheria hizi za Huduma, huenda ukakumbana na Maudhui ya Mtumiaji ambayo si sahihi au yasiyokubalika.  Bull City Learning inahifadhi haki, lakini haina jukumu, kufuatilia nyenzo zilizochapishwa kwenye maeneo ya hadharani ya huduma au kuwekea vikwazo au kumkataza mtumiaji kufikia Tovuti au kuchukua hatua nyingine mwafaka endapo mtumiaji atakiuka Sheria hizi za Huduma au atajihusisha katika shughuli yoyote inayokiuka haki za mtu au mhusika yeyote au shughuli yoyote tunayochukulia kuwa haramu, inayokosea, inayodhuru au ya nia mbaya. Ujumbe au barua pepe za moja kwa moja zilizotumwa baina yako na wanajamii wengine ambazo haziwezi kufikiwa na umma kwa ujumla au na jamii ya Bull City Learning community sisi tutazichukulia kuwa za siri/kibinafsi kwa kiwango kinachohitajika na sheria husika.  Bull City Learning itakuwa na haki ya kuondoa nyenzo zozote kama hizo ambazo kwa maoni yake zinakiuka, au zinadaiwa kukiuka, sheria au makubaliano haya au nyenzo zozote ambazo huenda zikawa na kukosea, au ambazo huenda zikakiuka haki, zinadhuru, au kutishia usalama wa watumiaji au wengine.  Matumizi bila idhini huenda yakapelekea kufunguliwa mashtaka ya kijinai na/au ya umma chini ya sheria za Serikali kuu, Jimbo na za mtaa.  Ukigundua matumizi mabaya ya Huduma zetu na/au Tovuti yetu, tafadhali WASILIANA NASI kwa anwani iliyotolewa hapa chini.

VIUNGO KWA TOVUTI NA/AU NYENZO NYINGINE

Kama sehemu ya Huduma, Bull City Learning huenda ikakupa viungo muhimu vya tovuti ya/za wahusika wengine ("Tovuti za Wahusika Wengine") na pia maudhui au vipengee vinavyomilikiwa au vinavyotoka kwa wahusika wengine ("Programu au Maudhui ya Wahusika Wengine").  Bull City Learning haina udhibiti juu ya Tovuti za Wahusika Wengine na Programu au Maudhui ya Wahusika Wengine au promosheni, nyenzo, maelezo, bidhaa au huduma zinazopatikana kwenye Tovuti hizi za Wahusika Wengine au Programu au Maudhui haya ya Wahusika Wengine.  

Tovuti hizo za Wahusika Wengine na Programu au Maudhui hayo ya Wahusika Wengine hayajachunguzwa, kufuatiliwa wala kukaguliwa kama ni sahihi, mwafaka, au kamili na Bull City Learning, na Bull City Learning haiwajibikii Tovuti zozote za Wahusika Wengine zinazofikiwa kwenye Tovuti au Programu au Maudhui yoyote ya Wahusika Wengine, yanayopatikana au kusakinishwa kupitia Tovuti, ikijumuisha maudhui, usahihi, ubaya wake, maoni, uaminifu, mazoea ya usiri au sera nyingine za au zilizo kwenye Tovuti za Wahusika Wengine au Programu au Maudhui ya Wahusika Wengine.  Kujumuisha, kuunganisha, au kuruhusu matumizi au usakinishaji wa Tovuti yoyote ya Wahusika Wengine au Programu au Maudhui yoyote ya Wahusika Wengine haiashirii kwamba imeidhinishwa au kuungwa mkono na Bull City Learning.  Ukiamua kuondoka kwenye Tovuti na utembele Tovuti za Wahusika Wengine au utumie Programu au Maudhui ya Wahusika Wengine, unafanya hivyo kwa shauri yako na unapaswa kufahamu kwamba sheria na sera zetu hazitumiki tena.  Unapaswa kupitia sheria na sera husika, pamoja na mazoea ya usiri na ukusanyaji data, za tovuti yoyote unayotembelea kupitia Tovuti hii au inayohusiana na programu zozote unazotumia au kusakinisha kutoka kwenye Tovuti.

MALALAMISHI YA HAKIMILIKI NA AJENTI WA HAKIMILIKI

(a) Kufungwa kwa Akaunti Zinazokiuka Maradufu.  Bull City Learning inaheshimu hakimiliki za wengine na inawaomba watumiaji wafanye hivyo pia.  Kulingana na kifungu cha 17 U.S.C. 512(i) cha Sheria ya Marekani ya Hakimiliki (kama ilivyorekebishwa), Bull City Learning imebuni na kutekeleza sera ambayo inaangazia ufungaji akaunti katika hali mwafaka za watumiaji wa Tovuti na/au Huduma ambao wanakiuka maradufu.  Bull City Learning inaweza kuwafungia ufikiaji washiriki au watumiaji ambao wanapatikana kutoa au kuchapisha maudhui ya wahusika wengine bila haki na ruhusa mwafaka.

(b) Ilani za Kuondoa Maudhui za DMCA.  Ikiwa wewe ni mmiliki hakimiliki au ajenti wa mmiliki hakimiliki na unaamini, kwa nia njema, kwamba nyenzo zozote zilizotolewa kwenye Tovuti zinakiuka hakilimiliki zako, unaweza kuwasilisha ilani kulingana na Sheria ya Hakimiliki ya Kidijitali ya Milenia (kama ilivyorekebishwa, tazama 17 U.S.C 512) ("DMCA") kwa kutuma maelezo yafuatayo kwa maandishi kwa ajenti mteule wa hakimiliki wa Bull City Learning kwa anwani: 102 City Hall Plaza, Suite 200, Durham, NC 27701.

 • Tarehe ya ilani yako;
 • Sahihi halisia au ya kielektroniki ya mtu aliyeidhinishwa kutenda kwa niaba ya mmiliki haki ambayo inadaiwa kukiukwa;
 • Maelezo kuhusu kazi yenye hakimiliki ambayo inadaiwa kukiukwa au, ikiwa kazi nyingi zenye hakimiliki katika tovuti moja mtandaoni zimejumuishwa kwenye ilani moja, ujumuishe orodha ya kazi hizo kwenye tovuti hiyo;
 • Maelezo ya nyenzo ambayo inadaiwa kukiukwa au inahusika katgika shughuli ya ukiukaji na maelezo tosha kutuwezesha kujua mahali tutaipata kazi huzika;
 • Maelezo tosha kumwezesha mtoa huduma kuwasiliana nawe, kama vile anwani, nambari ya simu, na/au anwani ya barua pepe;
 • Kauli kwamba una nia njema kwamba matumizi ya nyenzo kwa namna iliyoibua malalamishi hayajaidhinishwa na mmiliki hakimiliki, ajenti wake, au sheria; na,
 • Kauli kwamba maelezo yaliyo kwenye ilani ni sahihi, na chini ya sheria, kwamba umeidhinishwa kutenda kwa niaba ya mmiliki haki ambayo inadaiwa kukiukwa.

(c) Ilani za Kupinga. Ikiwa unaamini kwamba Maudhui yako ya Mtumiaji ambayo yameondolewa kwenye Tovuti hayakiuki, au kwamba una idhini kutoka kwa mmiliki hakimiliki, ajenti wa mmiliki hakimiliki, au kulingana na sheria, kuchapisha na kuyumia maudhui katika Maudhui yako ya Mtumiaji, unaweza kutuma ilani ya kupinga ambayo ina maelezo yafuatayo kwa ajenti wetu wa hakimiliki ukitumia maelezo ya mawasiliano yaliyobainishwa hapa juu.

 • Sahihi yako halisia au ya kielektroniki;
 • Maelezo ya maudhui ambayo yameondolewa na mahali ambapo maudhui hayo yalionekana kabla ya kuondolewa;
 • Kauli kwamba una nia njema kwamba maudhui yaliondolewa kutokana na hitilafu au maudhui kutambuliwa kimakosa; na
 • Jina, anwani, namabri ya simu na anwani yako ya barua pepe, kauli yako kwamba unatambua mamlaka ya mahakama ya kitaifa jimboni North Carolina na kauli kwamba utakubali kupokezwa hati za mashtaka kutoka kwa mtu aliyetoa ilani ya ukiukaji unaodaiwa.

Ilani ya kupiga ikipokewa na ajenti wa hakimiliki wa Bull City Learning, Bull City Learning huenda ikatuma nakala ya ilani hiyo ya kupinga kwa mhusika aliyeibua lalamishi na kumwarifu kwamba huenda ikarejesha maudhui hayo yaliyoondolewa baada ya siku 10 za kibiashara.  Isipokuwa mmiliki haki miliki atafungua kesi na kutafuta amri ya mahakama dhidi ya mtoa maudhui, mwanajamii au mtumiaji, (kwa hiari ya Bull City Learning) maudhui yaliyoondolewa huenda yakarejeshwa kwenye Tovuti baada ya siku 10 hadi 14 za kibiashara au zaidi baada ya kupokea ilani ya kupinga.

UTOAJI LESENI

Kwa kuchapisha Maudhui yoyote ya Mtumiaji kupitia Huduma, moja kwa moja unaipewa, na unawakilisha na kutoa hakikisho kwamba una haki ya kuipea, Bull City Learning leseni bila malipo, inayoweza kutolewa leseni ndogo, inayoweza kuhamishika, ya milele, isiyoweza kubatilishwa, isisyo ya kipekee, ya kote ulimwenguni ya kutumia, kuzalisha tena, kurekebisha, kuchapisha, kuorodhesha maelezo kuihusu, kuhariri, kutafsiri, kusambaza, kuiwasilisha hadharani, na kutegeneza kazi tohozi za Maudhui hayo yote ya Mtuamiaji na jina, sauti, na/au mfano wako kama ilivyo katika Maudhui yako ya Mtumiaji, ikiwa inahusika, kikamilifu au shemeu yake, ikijumuisha data zozote na zote amabzo zimeondolewa jina na zilizokadiriwa zilizotoholewa kwenye Maudhui ya Mtumiaji, kwa mfumo, midia, au teknolojia yoyote, iwe inajulikana sasa au kutengenezwa hapo baadaye, kwa matumizi yanayohusiana na Huduma.

MALI YA KIAKILI

Isipokuwa iwe imetajwa vinginevyo, Tovuti na Huduma ni mali yetu kibinafsi na msimbo chanzo, hifadhidata, utendaji, programu, miundo ya tovuti, sauti, video, maandishi, na picha zote kwenye Tovuti (kwa pamoja, "Maudhui" na alama za kibiashara, alama za huduma, na nembo zilizopo ("Alama") zinamilikiwa au kudhibitiwa nasi au kutolewa leseni nasi, na zinalindwa na sheria za hakimiliki na alama za kibiashara na sheria nyingine mbalimbali za hakimiliki na ushindani usio wa usawa za Marekani, mamlaka za kigeni, na sheria za kimataifa. Maudhui na Alama zinatolewa kwenye Tovuti na HUduma "KAMA ILIVYO" kwa maelezo na matumizi yako binafsi pekee. Isipokuwa kama ilivyobainishwa moja kwa moja katika Sheria hizi za Huduma, hakuna sehemu ya Tovuti na/au Huduma na hakuna Maudhui au Alama zinaweza kunakiliwa, kuzalishwa tena, kukadiriwa, kuchapishwa tena, kupakiwa, kuchapishwa, kuonyesha hadharani, kusimbwa, kutafsiriwa, kutumwa, kusambazwa, kuuzwa, kutolewa leseni, au vinginevyo kutumika kwa madhumuni yoyote ile ya kibiashara, bila kwanza kupata ruhusa ya moja kwa moja kwa maandishi. Hatutoi hakikisho kwamba Maudhui yataendeshwa bila kudakizwa au bila hitilafu au kwamba hitilafu zote zimesahihishwa. Aidha, hatutoi hakikisho kwamba Maudhui au vifaa, mfumo au mtandao wowote kwa ambao Maudhui yanatumika hayatakuwa na mapengo yoyote ya kudukuliwa au kushambuliwa.

Mradi tu unastahiki kutumia Tovuti na Huduma, unapewa leseni yenye kipimo ya kufikia na kutumia Tovuti na Huduma na ya kupakua na kuchapa nakala moja pekee ya sehemu yoyote ya Maudhui ambayo umefikia ipasavyo kwa matumizi ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara. Tunahifadhi haki zote amabzo haujapewa moja kwa moja kwenye Tovuti, Huduma, Maudhui na Alama. Sisi katika nyakati zote tunasalia na umiliki wa Maudhui kama ulivyoyapakuwa au kuyatumia na upakuaji wote wa matumizi yako ya Maudhui. Maudhui (na hakimiliki, na hakimiliki nyingine za aina yoyote ile katika Maudhui, ikijumuisha marekebisho yoyote yaliyofanywa) ni mali yetu na yatasalia kuwa mali yetu. Tunahifadhi haki ya kuwapea wahusika wengine leseni za kutumia Maudhui.

Kwa kutumia Tovuti na Huduma hizi, hapa unaiidhinisha Bull City Learning kutumia, kutumia tena, na kuwapea wengine haki za kutumia na kutumia tena, bila fidia nyingine yoyote ya ziada kwako, alama za kibiashara, majina ya kibiashara na nembo yako katika midia yoyote ambayo kwa sasa inajulikana au itakayotengenezwa katika siku zijazo. Matumizi hayo yatakuwa kwa namna ya kawaida na inayoeleweka kibiashara kwa madhumuni ya uuzaji, promosheni, na madhumuni mengine yanayohusiana na Tovuti na/au Huduma, na biashara yetu, na biashara nyingine, kwa nia njema kulingana na maamuzi yetu kuhusu kila matumizi.


BARUA PEPE HAIWEZI KUTUMIKA KUWASILISHA ILANI

Mawasiliano yanayofanywa kupitia barua pepe au mfumo wa ujumbe wa Huduma, hayatajumuisha ilani za kisheria zinazotumwa kwa Bull City Learning au kwa maafisa, waajiriwa, maajenti au wawakilishi wake wowote katika hali yoyote ambapo ilani kutumwa kwa Bull City Learning kunahitajika na mkataba au sheria au kanuni yoyote.

RIDHAA YA MTUMIAJI KUPOKEA MAWASILIANO KWA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Kwa madhumuni ya kimkataba, wewe (a) unatoa ridhaa ya kupokea mawasiliano kutoka kwa Bull City Learning kwa mfumo wa kielektroniki kupitia anwani ya barua pepe uliyowasilisha; na (b) unakubali kwamba Sheria zote za Huduma, makubaliano, ilani, ufichuaji, na mawasiliano mengine ambayo yanawasilishwa kwako na Bull City Learning kwa mfumo wa kieletroniki unatimiza mahitaji yoyote ya kisheria ambayo yangetimizwa na mawasiliano hayo kwa mfumo wa maandishi.  Yaliyotajwa hapa juu hayaathiri haki zako ambazo haziwezi kuondolewa. Pia tunaweza kutumia anwani yako ya barua pepe, kukutumia ujumbe mwingine ikiwa ni pamoja na maelezo kuhusu Bull City Learning na ofa maalum. Unaweza kujiondoa kupokea barua pepe za aina hiyo kwa kubadilisha mipangilio ya akaunti yako kwa kuwasiliana na usaidizi wa wateja kwa anwani support@BullCityLearning. 

Kujiondoa kunaweza kukuzuia kupokea ujumbe unaohusiana na Bull City Learning au ofa maalum.


UREKEBISHAJI WA SHERIA ZA HUDUMA

Tunaweza kurekebisha Sheria hizi za Huduma wakati wowote na tutasasisha Sheria hizi za Huduma endapo kutakuwa na marekebisho yoyote kama hayo.  Ni jukumu lako pekee yako kukagua Tovuti mara kwa mara ili kuona kama kuna mabadiliko katika Makubaliano.  Ukiendelea kutumia Tovuti, unaashiria kwamba unakubaliana na marekebisho yetu kwenye Sheria hizi za Huduma.  Hata hivyo, tutakuarifu kuhusu mabadiliko makubwa kwenye sheria kwa kuchapisha ilani kwenye ukurasa wetu wa kwanza na/au kutuma barua pepe kwa anwani ya barua pepe ambayo ulitupatia baada ya kujisajili. Kwa sababu hii ya ziada, unapaswa kuhakikisha kwamba maelezo yako ya mawasiliano na wasifu ni ya sasa. Mabadiliko yoyote yanayofanyiwa Sheria hizi (kando na kama ilivyobainishwa katika aya hii) au uondoaji wa haki za Bull City Learning hayatakuwa halali au hayatatumika isipokuwa kuwe na makubaliano kwa maandishi yaliyo na sahihi halisia ya afisa wa Bull City Learning. Uondoaji au urekebishaji unaodaiwa kufanywa kwenye Makubaliano haya na Bull City Learning kupitia mawasiliano kwa simu au barua pepe yautakuwa halali.

UDHIBITI TOVUTI

Bull City Learning inahifadhi haki, lakini haina jukumu la: (1) kufuatilia Tovuti kuona kama kuna ukiukaji wa Sheria hizi za Huduma; (2) kuchukua hatua mwafaka ya kisheria dhidi ya mtu yeyote ambaye, kwa hiari yetu pekee, anakiuka sheria na Sheria hizi za Huduma, ikijumuisha lakini sio tu, kuripoti mtumiaji huyo kwa mamlaka za kutekeleza sheria; (3) kwa hiari yetu pekee na bila kikwazo, kukataza, kuwekea kikwazo cha kufikia, upatikanaji wa, au kulemaza (kwa kiwango kinachowezekana kiteknolojia) Michango yako yoyote au sehemu yake; (4) kwa hiari yetu pekee na bila kikwazo, kutoa ilani, au dhima, ya kuondoa kwenye Tovuti au vinginevyo kulemaza faili na maudhui ambayo ukubwa wake umepitisha kiwango au ambayo kwa njia yoyote ni mzigo mzito kwa mifumo yetu; na (5) vinginevyo kudhibiti Tovuti kwa namna ambayo imebuniwa kulinda haki na mali yetu na ili kuwezesha utendakazi mwafaka wa Tovuti.

MUHULA NA USITISHAJI

Sheria hizi za Huduma zitasalia kutumika kikamilifu unapotumia Tovuti, na zitasalia kutumika mpaka wakati (i) utatuarifu kwa maandishi kwamba unataka kufunga akaunti yako (ii) utakosa kuambatana na sheria na masharti yoyote ya Sheria hizi za Huduma, au (iii) tutaahirisha akaunti yako. BILA KUWEKEA KIKWAZO SEHEMU NYINGINE YOYOTE YA SHERIA HIZI ZA HUDUMA, TUNAHIFADHI HAKI, KWA HIARI YETU PEKEE NA BILA KUTOA ILANI AU DHIMA, YA KUKATAZA UFIKIAJI NA MATUMIZI YA TOVUTI (IKIJUMUISHA KUZUILIA ANWANI FULANI ZA IP), KWA MTU YEYOTE KWA AJILI YA SABABU YOYOTE AU BILA SABABU, IKIJUMUISHA LAKINI SIO TU UKIUKAJI WA UWAKILISHI, HAKIKISHO, AU MAKUBALIANO YOYOTE YALIYO KATIKA SHERIA HIZI ZA HUDUMA AU YA SHERIA AU KANUNI ZOZOTE HUSIKA. TUNAWEZA KUSITISHA MATUMIZI AU USHIRIKI WAKO KATIKA TOVUTI AU KUFUTA AKAUNTI YAKO NA MAUDHUI AU MAELEZO YOYOTE AMBAYO UMECHAPISHA WAKATI WOWOTE, BILA ONYO, KWA HIARI YETU PEKEE.

Tukifunga au kuiahirisha akaunti yako kwa ajili ya sababu yoyote, leseni ambazo ulipewa na Sheria hizi za Huduma zitasitishwa maramoja na unakubali kusitisha ufikiaji na matumizi yote ya Tovuti na/au Huduma. Umepigwa marufuku ya kusajili na kuunda akaunti mpya ukitumia jina lako, jina bandia, au jina la mhusika mwingine yeyote, hata kama unatenda kwa niaba ya mhusika huyo mwingine. Kando na kufunga au kuahirisha akaunti yako, tunahifadhi haki ya kuchukua hatua mwafaka ya kisheria, ikijumuisha lakini sio tu kufungua kesi ya umma, kijinai, na ya kupata amri ya mahakama.

MAREKEBISHO NA KUDAKIZWA

Tunahifadhi haki ya kubadilisha, kurekebisha, au kuondoa maudhui ya Tovuti wakati wowote kwa hiari yetu pekee bila ilani. Hata hivyo, hatuna jukumu la kusasisha maelezo yoyote kwenye Tovuti yetu. Pia tunahifadhi haki ya kubadilisha au kusitisha Tovuti nzima au sehemu yake wakati wowote bila ilani. Hatutakuwa na dhima kwako au kwa mhusika mwingine yeyote kwa ajili ya rekebisho lolote, badiliko la bei, uahirishaji, au usitishaji Tovuti.

Hatuwezi kutoa hakikisho kwamba Tovuti itapatikana nyakati zote. Huenda tukakumbwa na matatizo ya mitambo, programu, au matatizo mengine au tukahitaji kufanya udumishaji unaohusiana na Tovuti, utakaopelekea kudakizwa, ucheleweshwaji, au hitilafu. Tunahifadhi haki ya kubadilisha, kurekebisha, kusasisha, kusitisha, au vinginevyo kubadilisha Tovuti wakati wowote kwa ajili ya sababu yoyote bila kukutumia ilani. Unakubali kwamba hatuna dhima yoyote ile kwa ajili ya hasara, au usumbufu unaosababishwa na wewe kutoweza kufikia au kutumia Tovuti wakati Tovuti haipeperushwi au imesitishwa. Hakuna chochote katika Sheria hizi za Huduma kitakachochukuliwa kuashiria kwamba tuna jukumu la kudumisha na kusaidia Tovuti au kufanya marekebisho, masasisho, au matoleo yoyote yanayohusiana na Tovuti.

USAHIHISHAJI

Kwenye Tovuti, huenda kukawa na maelezo ambayo yana hitilafu, kasoro, au makosa ya kimaandishi, ikijumuisha maelezo, bei, upatikanaji, na maelezo mengine mbalimbali. Tunahifadhi haki ya kusahihisha hitilafu, kasoro, au makosa yoyote na kubadilisha au kusasisha maelezo yaliyo kwenye Tovuti na/au Huduma wakati wowote bila kwanza kukutumia ilani.

KANUSHO NA HAKIKISHO

TOVUTI NA HUDUMA ZINATOLEWA "KAMA ILIVYO", BILA HAKIKISHO LA AINA YOYOTE. BILA KUJALI YALIYOTAJWA HAPA JUU, Bull City Learning MOJA KWA MOJA INAKANUSHA HAKIKISHO ZOTE, ZA MOJA KWA MOJA, ZILIZODOKEZWA AU ZILIZOPO, KUHUSIANA NA HUDUMA IKIJUMUISHA LAKINI SIO TU HAKIKISHO ZA KIBIASHARA, KUFAA KWA DHUMUNI FULANI, UDHAMINI, USAHIHI NA KUTOKIUKWA KWAKE. BILA KUJALI YALIYOTAJWA HAPA JUU, Bull City Learning HAITOI UKAKIKISHO WALA UWAKILISHI KWAMBA UFIKIAJI AU UENDESHAJI WA HUDUMA HAUTADAKIZWA WALA KUKOSA HITILAFU. UNAWAJIBIKA KIKAMILIFU KWA HASARA ZINAZOTOKANA NA UPAKUAJI WAKO NA/AU MATUMIZI YAKO YA FAILI, MAELEZO, MAUDHUI AU NYENZO NYINGINE ZILIZOTOLEWA KWENYE TOVUTI. BAADHI YA MAMLAKA ZINAWEKEA VIKWAZO AU HAZIRUHUSU MAKANUSHO YA HAKIKISHO, KWA HIVYO HUENDA KIFUNGU HIKI KIKAKOSA KUKUATHIRI WEWE.

KIPIMO CHA HASARA; KIBALI

KWA KIWANGO KINACHORUHUSIWA NA SHERIA HUSIKA, HAKUNA WAKATI WOWOTE AMBAPO Bull City Learning, WASHIRIKA, WAKURUGENZI, AU WAAJIRI, AU WANAOIPA LESENI AU WABIA WAKE, WATAKUWA NA DHIMA KWAKO KWA AJILI YA UPOTEZAJI WOWOTE WA FAIDA, MATUMIZI,  AU DATA, AU KWA AJILI YA HASARA ZOZOTE ZA KIAJALI, ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA, MAALUM, ZINAZOTOKANA NA JAMBO NYINGINE AU ZA KIPEKEE, BILA KUJALI ZINAVYOIBUKA, ZINAZOTOKANA NA (A) MATUMIZI, UFICHUAJI, AU UONYESHAJI WA MAUDHUI YAKO YA MTUMIAJI; (B) MATUMIZI YAKO AU WEWE KUTOWEZA KUTUMIA HUDUMA; (C) HUDUMA JUMLA AU PROGRAMU AU MIFUMO INAYOWEZESHA HUDUMA KUPATIKANA; AU (D) AU UTANGAMANO MWINGINE WOWOTE NA Bull City Learning AU MTUMIAJI MWINGINE YEYOTE WA HUDUMA, IWE INATEGEMEA HAKIKISHO, MKATABA, UKIUKAJI (IKIJUMUISHA UTELEKEZAJI) AU NADHARIA NYINGINE YOYOTE YA KISHERIA, NA KANA KWAMBA Bull City Learning IMEFAHAMISHWA KUHUSU UWEZEKANO WA HASARA HIYO AU LA, NA HATA KAMA SULUHU ILIYOBAINISHWA HAPA IMEPATIKANA KUTOFAULI KATIKA KUSUDI LAKE.  BAADHI YA MAMLAKA ZINAWEKEA VIKWAZO AU HAZIRUHUSU MAKANUSHO YA DHIMA, KWA HIVYO HUENDA KIFUNGU HIKI KIKAKOSA KUKUATHIRI WEWE.

Ikiwa una mgogoro na mtumiaji mmoja au zaidi unatuondoa (pamoja na maafisa, wakurugenzi, maajenti, kampuni zetu tanzu, biashara zetu na waajiriwa wetu) kwenye madai, na hasara (halisi na zinazotokana na jambo lingine) za kila aina, zinazojulikana na zisizojulikana, zinazotokana na migogoro hiyo au kuhusiana na migogoro hiyo kwa njia yoyote.  Ikiwa wewe ni makaazi wa California, unaondoa sheria ya California Civil Code §1542, ambayo inasema: "Kibali jumla hakitumiki kwa madai ambayo mtoa mkopo hayajui au hafikirii kuwa yapo ili kujinufaisha wakati wa kuidhinisha kibali, ambapo ikiwa aliyafahamu yangeathiri makubaliano yake na mkopaji."

KUONDOLEWA LAWAMA

Unakubali kututetea, kutuondolea lawama, na kutuchukua bila makosa, ikijumuisha kampuni zetu tanzu, washirika wetu, na maafisa, maajenti, wabia, na waajiriwa wetu wote, dhidi ya hasata, dhima, au madai yoyote, ikijumuisha ada na gharama za wakili, yanayofanywa na mhusika mwingine yeyote au yanayoibuka kutokana na: (1) Maudhui yako ya Mtumiaji; (2) matumizi ya Tovuti na/au Huduma; (3) Ukiukaji wa Sheria hizi za Huduma; (4) ukiukaji wowote wa uwakilishi na hakikisho zako ulizobainisha katika Sheria hizi za Huduma; (5) ukiukaji wako wa haki za mhusika mwingine, ikijumuisha lakini sio tu, hakimiliki; au (6) tendo nyingine lolote halifu dhidi ya mtumiaji mwingine yeyote wa Tovuti ambaye unahusiana naye kupitia Tovuti. Bila kujali yaliyotajwa hapa juu, kwa gharama yako, tunahifadhi haki ya kuchukua utetezi na udhibiti wa suala lolote kwa ambalo unahitajika kutuondolea lawama, na, kwa gharama yako, unakubali kushirikiana na utetezi wetu kwa ajili ya madai hayo. Tutatumia juhudi mwafaka ili kukuarifu kuhusu dai, mashtaka, au kesi yoyote kama hiyo ambayo iko chini ya uondoaji lawama huu baada ya kufahamishwa kuihusu. Unakubali kutufidia, baada ya sisi kudai, gharama zozote za utetezi tunazogharimia na malipo yoyote tunayofanya au hasara zinazotukumba, iwe ni katika uamuzi wa mahakama au makubaliano.

Ikiwa sheria inakuzuia kuwa na jukumu la uondoaji lawama lililo hapa juu, basi unakubali, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria, dhima yote kwa madai, mashtaka, dhima, na gharama zote (ikijumuisha ada za wakili, gharama na ada za shahidi wa kitaalamu) ambazo zinatajwa kuwa suala la jukumu la uondoaji lawama lililo hapa juu. 

DATA ZA MTUMIAJI

Tutahifadhi data fulani unazoweka kwenye Tovuti kwa madhumuni ya kudhibiti utendakazi wa Tovuti, na pia data zinazohusiana na matumizi yako ya Tovuti. Ingawa tunaweka hifadhirudufu za data mara kwa mara, unawajibikia data zote unazoweka kwenye Tovuti au zinazohusiana na shughuli zozote unazoendesha unapotumia Tovuti. Unakubali kwamba hatutakuwa na dhima kwako kwa ajili ya upotezaji au uharibikaji wowote wa data zozote kama hizo, na hapa unaondoa haki yoyote ya kuchukua hatua dhidi yetu inayotokana na upotezaji au uharibikaji wowote kama huo wa data hizo.

UTUMAJI UJUMBE BAINA YA WATUMIAJI

Matumizi yako ya Tovuti huenda yakahusisha Huduma zinazowezesha mawasiliano baina yako na watumiaji wengine kupitia utumaji ujumbe wa SMS/MMS na mbinu nyingine za mawasiliano za kielektroniki. Idadi ya ujumbe unaopokea, inatofautiana kulingana na Huduma unazotumia na kiwango cha utangamano wako na watumiaji wengine wa Tovuti.

Ada za ujumbe na data huenda ikatozwa kwa kila ujumbe wa arafa unaotuma au kupokea, kama ilivyobainishwa katika mpango wako wa huduma za simu, kando na ada zozote husika za ulandaji.  Tafadhali wasiliana na mtoa huduma ya simu kwako ili kupata mipango na maelezo ya bei. Isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo chini ya makubaliano ya usajili au huduma za kitaalamu ambayo tumeidhinisha, hatutozi na hatutatoza ada ya kando kwa ajili ya kutuma ujumbe.

Unawakilisha kwamba wewe ndiye unamiliki akaunti ya nambari ya simu unayopeana.  Unaweza kuiarifu Bull City Learning kuhusu mabadiliko ya nambari kwa kuwasiliana na Bull City Learning ukitumia anwani ya KUWASILIANA NASI iliyotolewa hapa chini.

Ikiwa, kwa wakati wowote, ungependa kuacha kupokea ujumbe wa arafa, Bull City Learning itakupa nambari ambayo utaitumia ujumbe wa STOP na hautapokea ujumbe kutoka kwa nambari hiyo tena.  Kisha utapokea thibitisho la kujiondoa kwako ili kutopokea ujumbe wa arafa. Pia unaweza kuwasiliana na Bull City Learning ukitumia anwani ya KUWASILIANA NASI iliyotolewa hapa chini na hautapokea tena ujumbe kutoka kwa anwani hiyo.

Unakubali kuiondolea lawama Bull City Learning kikamilifu kwa madai, gharama, na hasara zote zinazoibuka kutokana au kuhusiana na ukosefu wako wa kuiarifu Bull City Learning ukibadilisha nambari yako ya simu, ikijumuisha, lakini sio tu, madai, gharama, na hasara zote zinazohusiana au kuibuka chini ya Sheria ya Ulindaji Wateja kwa Simu (kama ilivyorekebishwa). 

HAKUNA UWAKALA

Hakuna mtumiaji kwenye Tovuti hii au wa Huduma ana idhini ya kufanya mkataba, makubaliano, hakikisho au uwakilisho kwa niaba yetu au kutengeneza jukumu, lilioonyeshwa au kudokezwa, kwa niaba yetu. Hautatenda wala kujiwasilisha kama ajenti wetu, mbia wetu, au mfanyibiashara mwenzetu.

WATUMIAJI NA WAKAAZI WA CALIFORNIA

Ikiwa lalamishi lolote halijasuluhiswha kwa njia ya kuridhisha, unaweza kuwasiliana na Kitengo cha Usaidizi wa Malalmishi cha Idara ya Huduma za Wateja ya Idara ya California ya Maslahi ya Wateja kwa maandishi ukitumia anwani Department of Consumer Affairs, Consumer Information Division, 1625 North Market Blvd., Suite N 112, Sacramento, CA 95834 or by telephone at (800) 952-5210.

USULUHISHAJI NA UONDOAJI LALAMISHI LA PAMOJA

MGOGORO, SAKATA, AU DAI LOLOTE LINALOIBUKA KUTOKANA, AU KUHUSIANA NA MAKUBALIANO HAYA, IKIJUMUISHA UKIUKAJI, USITISHAJI, AU UHALALI WAKE, HATIMAYE LITASULUHISHWA KWA USULUHISHAJI. JOPO HILO LITAKUWA NA NGUVU YA KUTOA UAMUZI KUHUSU CHANGAMOTO YOYOTE KWENYE MAMLAKA YAKE BINAFSI AU KWENYE UHALALI AU UWEZO WA KUTEKELEZA SEHEMU YOYOTE YA MAKUBALIANO YANAYOSULUHISHWA. WAHUSIKA WANAKUBALI KUSULUHISHA KIBINAFSI KWA KILA TUKIO BINAFSI, NA KWAMBA MAKUBALIANO HAYA YA KUSULUHISHA HAYARUHUSU USULUHISHAJI WA PAMOJA AU MADAI YOYOTE KAMA MLALAMISHI AU MMOJA KWENYE KUNDI KATIKA KUNDI LOLOTE AU KESI WAKILISHI YA USULUHISHAJI. JOPO LA USULUHISHAJI HALIWEZI KUJUMUISHA MADAI YA ZAIDI YA MTU MMOJA, NA HALIWEZI KUSIMAMIA AINA YOYOTE YA KESI YA UWAKILISHI AU YA PAMOJA. ENDAPO MARUFUKU YA USULUHISHAHI WA PAMOJA ITAONEKANA KUWA SI HALALI AU HAIWEZI KUTEKELEZEKA, BASI SEHEMU ZINAZOSALIA ZA MAKUBALIANO YA USULUHISHAJI ZITAENDELEA KUTUMIKA.

BILA KUJALI YALIYOTAJWA HAPA JUU, WAHUSIKA WANAONDOA HALI YOYOTE YA KUWEKA MADAI YOYOTE DHIDI YA MHUSIKA YULE MWINGINE KAMA MWAKILISHI AU MSHIRIKI KATIKA MASHTAKA YOYOTE YA PAMOJA AU YA UWAKILISHI. KWA KIWNGO AMBACHO KILA MHUSIKA ANARUHUSIWA NA SHERIA AU MAHAKAMA KUENDELEA NA MASHATAKA YA PAMOJA AU UWAKILISHI DHIDI YA MWINGINE, WAHUSIKA HAO WANAKUBALIANA KWAMBA: (I) MHUSIKA ANAYETANGULIA HATAKUWA NA HAKI YA KUFIDIA ADA NA GHARAMA ZA WAKILI ZINAZOHUSIANA NA KESI YA PAMOJA AUA UWAKILISHI (BILA KUJALI KIFUNGU KINGINE CHOCHOTE KATIKA MAKUBALIANO HAYA); NA (II) MHUSIKA ANAYEANZISHA AU KUSHIRIKI KAMA MMOJA KWENYE KUNDI HATAWASILISHA DAI AU VINGINEVYO KUSHIRIKI KATIKA KUREJESHA GHARAMA ZINAZOPATIKANA KUPITIA KESI YA PAMOJA AU UWAKILISHI.

SHERIA JUMLA

Sehemu yoyote ya Makubaliano haya ikipatikana kuwa si halali au haiwezi kutekelezeka, sehemu hiyo ya Makubaliano itachukuliwa kulingana na sheria husika.  Sehemu zinazosalia zitasalia kutumika kikamilifu. Ukosefu wowote wa Bull City Learning wa kutekeleza sehemu yoyote ya Makubaliano haya haitachukuliwa kuwa tumeondoa haki yetu ya kutekeleza sehemu hiyo.  Haki zetu chini ya Makubaliano haya zitasalia hata Makubaliano haya yakisitishwa.

Unakubali kwamba hatua yoyote inayohusiana au kuibuka kutokana na uhusiano wako na Bull City Learning ni lazima ianzishwe ndani ya mwaka MMOJA baada ya hatua hiyo kujitokeza.  Vinginevyo, hatua hiyo imefungiwa daima.

Sheria hizi za Huduma na matumizi yako ya Tovuti yanatawaliwa na sheria za kitaifa za Marekani na sheria za Jimbo la North Carolina, bila kujali vifungu vya ukinzani na sheria.

Bull City Learning, inaweza kupeana jukumu la Sheria hizi za Huduma na/au Sera ya Usiri ya Bull City Learning, zote kikamilifu au sehemu yake, kwa mtu au mhusika yeyote wakati wowote kwa idhini yako au bila idhini yako. Hauwezi kupatiana au kupeana jukumu la haki au majukumu yoyote chini ya Sheria hizi za Huduma au Sera ya Usiri bila kibali cha awali kwa maandishi cha Bull City Learning, na upatianaji au upeanaji jukumu wowote unaoufanya si halali.

UNAKIRI KWAMBA UMESOMA SHERIA HIZI ZA HUDUMA, UMEELEWA SHERIA HIZI ZA HUDUMA, NA UTAFUNGWA NA SHERIA NA MASHARTI HAYA. AIDHA UNAKIRI KWAMBA SHERIA HIZI ZA HUDUMA PAMOJA NA SERA YA USIRI ZINAWAKILISHA KAULI KAMILI NA YA KIPEKEE YA MAKUBALIANO BAINA YETU NA KWAMBA ZINAPIKU PENDEKEZO AU MAKUBALIANO YOYOTE YA AWALI KWA MATAMSHI AU MAANDISHI, NA MAWASILIANO MENGINE YOYOTE BAINA YETU YANAYOHUSIANA NA MASUALA YA MAKUBALIANO HAYA.

GHARAMA NA ADA ZA WAKILI

Tukitumia huduma za wakili ili kukusanya fedha zozote zinazodaiwa kutoka kwako au ili kukufungulia mashtaka yoyote, yanayoibuka au kuhusiana na Sheria hizi za Huduma, na tufaulu kupata maamuzi tuliyotaka kupata, unakubali kulipa na kutoa fidia bila kuchelewa ada zozote na zote za wakili, iwe ni katika maelewano au usuluhishaji, au kwa rufaa.

WASILIANA NASI

Ili kusuluhisha lalamishi kuhusiana na Tovuti au ili kupokea maelezo kuhusiana na Tovuti, tafadhali wasiliana nasi kwa anwani: [email protected].