Bull City Learning, Inc.
Sera ya Usiri
Haki na Ufichuaji jimboni California
Bull City Learning, Inc., ikijumuisha washirika wake ("Bull City Learning", "sisi", "yetu", au "zetu") wanajitahidi kudumisha ulinzi imara wa usiri wako, iwe ni wa kibinafsi au kwa niaba ya mhusika mwingine ("wewe", "mteja", "mtumiaji" au "yako/zako").
Kando na haki zilizoorodheshwa katika Sera yetu ya Usiri ambazo zinatumika kwa watumiaji wote, katika baadhi ya matukio, wakaazi wa California huenda wakawa na haki zifuatazo kuhusu maelezo fulani yaliyokusanywa, kutumika, na kushirikiwa kulingana na Sera yetu ya Usiri.
Madhumuni ya matumizi hapa, neno "Tovuti" linarejelea tovuti yetu, blogi zetu, akaunti zetu za mitandao ya kijamii, au programu zetu kwa ambazo huduma ya Bull City Learning inaweza kufikiwa ambapo watumiaji wanaweza kutazama tovuti na kujisajili kutumia programu, bidhaa, na huduma zetu ("Huduma," kwa pamoja ni "Huduma").
Tafadhali chukua muda kusoma kwa makini Sera hii ya Usiri kwani usiri wako ni muhimu kwetu. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu jinsi tunavyokusanya, tunavyotumia, tunavyolinda, au vinginevyo tunavyoshughulikia Maelezo yako ya Kibinafsi (kama ilivyoelezewa hapa chini), tafadhali wasiliana nasi ukitumia maelezo ya mawasiliano yaliyo hapa chini.
Isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo katika Sera hii ya Usiri, maneno yaliyotumiwa katika Sera hii ya Usiri yana maana sawia na ilivyotumika katika Sheria zetu za Huduma. Kwa kutumia Huduma, unatoa ridhaa ya sisi kukusanya, kuhifadhi, kutumia na kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi chini ya masharti yaliyobainishwa hapa.
Tunakusanya na kushiriki maelezo kama ilivyoelezwa katika Sehemu ya I na Sehemu ya II ya Sera yetu ya Usiri. Kama inavyotumika kwa kategoria za maelezo yaliyobainishwa katika Sheria ya 2018 ya California ya Usiri wa Mtumiaji:
Sehemu ya 1798.83 ya Sheria ya California ya Umma inaruhusu wateja wetu ambao wanaishi California kuomba maelezo fulani kuhusu ufichuaji wetu maelezo ya kibinafsi kwa wahusika wengine kwa madhumuni yao ya moja kwa moja ya uuzaji. Hatushiriki maelezo ya kibinafsi ya wateja wetu na wahusika wengine ambao hatuhusiani kwa ajili ya madhumuni yao binafsi ya uuzaji wa moja kwa moja.
Sehemu ya 22581 ya Sheria ya California ya Biashara na Taaluma inakuruhusu, ikiwa wewe ni mkaazi wa California mwenye umri wa chini ya miaka 18, kutazama, kurekebisha, au kuondoa maelezo uliyotoa au uliyochapisha hadharani, kwa kuingia kwenye akaunti yako au bidhaa au huduma nyingine na kuhariri/kuondoa maelezo yako ya kibinafsi. Utahitaji nenosiri lako ili kuingia kwenye akaunti yako ya kibinafsi. Pia unaweza kututumia ombi kwa barua pepe au maandishi na kutuomba tuondoe maudhui fulani yaliyochapishwa ukitumia anwani iliyo katika sehemu ya Maelezo ya Mawasiliano katika hati hii.
Tutafurahia kukagua, kusasisha, au kuondoa maelezo na/au maudhui kama inavyohitajika. Mabaki ya nakala za maelezo au maudhui ambayo yameondolewa kutoka kwenye akaunti yako na/au jukwaa letu huenda yakasalia katika mifumo yetu ya hifadhirudufu kwa takriban mwezi mmoja. Bado huenda tukasalia kuhifadhi maelezo yako ili kusuluhisha migogoro, kutekeleza makubaliano baina yetu na watumiaji, au kuambatana na mahitaji ya kisheria; katika tukio hili, maelezo yako ya kibinafsi yatazuiliwa kutumika kwa madhumuni mengine yoyote.
Sehemu ya 22575(b) ya Sheria ya California ya Biashara na Taaluma inawaruhusu wateja wetu wanaoishi California kufahamishwa jinsi ya kukabiliana na mipangilio ya kivinjari wavuti ya "Kutofuatiliwa". Kwa sababu Kutofuatiliwa ni kipengee msingi kinachotengenezwa, hatuchukui hatua za kukabiliana na mipangilio ya Kutofuatiliwa, na badala yake tunaambatana na sheria zilizobainishwa katika Sera hii ya Usiri. Ikiwa ungependa kujua mengi zaidi kuhusu Kutofuatiliwa, unaweza kupata kiungo kifuatacho kuwa muhimu: http://www.allaboutdnt.com/.
Maombi yoyote ya kutumia haki za Watumiaji yanaweza kutumwa kwa Mmiliki kupitia maelezo ya mawasiliano yaliyo hapa chini. Maombi haya yanaweza kutumwa bila malipo na yatashughulikiwa na Mmiliki punde iwezekanavyo na kila wakati ndani ya mwezi mmoja. Kwa maombi yote, tafadhali taja kwamba ombi hilo linahusiana na "Haki za Usiri Jimboni California" na upatiane jina lako, anwani ya mtaa wako, mji wako, jimbo lako, msimbo wako wa zip, na anwani yako ya barua pepe au nambari yako ya simu ambayo inaweza kutumika kuwasiliana nawe.
Kabla ya tujibu ombi lako, sheria za California inatuhitaji kuthibitisha utambulisho wako tukitumia maelezo yako ya kibinafsi. Ikiwa sisi (au wahusika wengine tunaowahusisha ili kutusaidia) hatutaweza kuthibitisha ombi lako, tutwawasiliana nawe ili kupata maelezo zaidi. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha utambulisho wako baada ya jaribio kwa nia njema, huenda tukakataa ombi hilo na, ikiwa hivyo, tutaelezea msingi wa sisi kukataa.
Unaweza kumteua mtu kuwasilisha maombi na kutenda kwa niaba yako kama ajenti aliyeidhinishwa. Ili kufanya hivyo, ni lazima utupatie ruhusa kwa maandishi ili tumruhusu ajenti wako aliyeidhinishwa atende kwa niaba yako na, panapofaa, kukubali maelezo kukuhusu. Vyovyote vile, wewe na/au ajenti wako aliyeidhinishwa ni lazima mtupatie maelezo tosha ambayo yatatuwezesha kuthibitisha utambulisho wako.
Bull City Learning, Inc.
[email protected]