Unaweza kuingiza IA Watch kwenye kazi yako kwa njia nyingi, ikiwemo:
Video zote zinatokana na mwongozo uliothibitishwa wa WHO na umetengenezwa kwa msaada wa bodi ya ushauri ya afya iliyo na wataalam wa kimataifa na watendaji wa ndani wa maeneo husika.
Video zote zinapatikana kwa Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili na Hausa, na lugha zingine kuongezwa hivi karibuni.
Kama sehemu ya ubunifu unaojali mahitaji ya watumiaji, Taasisi ya BCL ilifanya ve research to identify the current challenges and content priorities of the target audience and key stakeholders.
Mahojiano ya kina, mahojiano ya vikundi, na vipindi ya kufanya kazi na makundi ya watumiaji Tanzania. Kulingana na na haya na miongozo ya chanjo iliyopo ambayo imewekwa na WHO, orodha ya mada zenye umuhimu za video zilianzishwa na kupitishwa na walengwa.
Baada ya kuthibitishwa, kila mada ya video ilitafitiwa kwa kutumia mwongozo wa WHO na mahoiano na wataalam wa mada husika. Video zilipitiwa na kuboreshwa na jopo la wataalam wa mada husika, pamoja na wadau kutoka Wizara ya Afya Tanzania. Mchakato wa uhariri na mapitio ulifanywa kwa uhuru, bila kuwa na kuingiliwa kokote zaidi ya kule kulikolezewa hapo juu.
Watu wafuatao wamepitia nyaraka za mafunzo na kutoa mwongozo kuhusu mada za mafunzo ya chanjo.
Immunization Academy ni mpango wa mafunzo duniani kote unaoongozwa na wataalam wa mafunzo wa Taasisi ya BCL Institute. Mpango huu unadhaminiwa na msaada kutoka kwa mfuko wa Bill na Melinda Gates na umeundwa kwa kutumia mwongozo uliothibitishwa na WHO, ukijumuisha mafunzo kwa mameneja wa ngazi ya kati(MLM) na Chanjo Kivitendo (IIP).