Bull City Learning, Inc.
Sera ya Usiri
Haki na Ufichuaji katika Mamlaka Nje ya Marekani
Bull City Learning, Inc., ikijumuisha washirika wake ("Bull City Learning", "sisi", "yetu", au "zetu") wanajitahidi kudumisha ulinzi imara wa usiri wako, iwe ni wa kibinafsi au kwa niaba ya mhusika mwingine ("wewe", "mteja" au "mtumiaji" au "yako/zako").
Kando na haki zilizoorodheshwa katika Sera yetu ya Usiri ambazo zinatumika kwa watumiaji wote, katika baadhi ya matukio, wakaazi kutoka nje ya Marekani huenda wakawa na haki zifuatazo kuhusu maelezo fulani yaliyokusanywa, kutumika, na kushirikiwa kulingana na Sera yetu ya Usiri.
Madhumuni ya matumizi hapa, neno "Tovuti" linarejelea tovuti yetu, blogi zetu, akaunti zetu za mitandao ya kijamii, au programu zetu kwa ambazo huduma ya Bull City Learning inaweza kufikiwa ambapo watumiaji wanaweza kutazama tovuti na kujisajili kutumia programu, bidhaa, na huduma zetu ("Huduma," kwa pamoja ni "Huduma").
Tafadhali chukua muda kusoma kwa makini sera hii ya Haki na Ufichuaji katika Mamlaka Nje ya Marekani na pia Sera yetu ya Usiri, kwani usiri wako ni muhimu kwetu. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu jinsi tunavyokusanya, tunavyotumia, tunavyolinda, au vinginevyo tunavyoshughulikia Maelezo yako ya Kibinafsi (kama ilivyoelezewa hapa chini), tafadhali wasiliana nasi ukitumia maelezo ya mawasiliano yaliyo hapa chini.
Isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo katika sera hii ya Haki na Ufichuaji katika Mamlaka Nje ya Marekani, maneno yaliyotumiwa katika Sera hii ya Usiri yana maana sawia na ilivyotumika katika Sera yetu ya Usiri. Kwa kutumia Huduma, unatoa ridhaa ya sisi kukusanya, kuhifadhi, kutumia na kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi chini ya masharti yaliyobainishwa hapa.
Tunasindika tu Maelezo yako ya Kibinafsi ambapo tunaweza kutegemea misingi ya kisheria kuweza kufanya hivyo. Tunasindika Maelezo yako ya Kibinafsi kwa ajili ya utekelezaji Huduma zetu, ili kutoa usaidizi kuhusu bidhaa zetu, au kwa ajili ya kipengele kingine unachoomba au kuwezesha. Hii inajumuisha, kwa mfano, kutumia Maelezo yako ya Kibinafsi kusimamia akaunti yako, kutoa promosheni ambazo umejisajili kushiriki; kuwezesha ununuzi ulioufanya, kuwezesha utendakazi wa programu, kutoa huduma ya wateja kote ulimwenguni, au kutoa huduma nzuri ya matumizi ya watumiaji kwa kutumia teknolojia za kukabiliana na ulaghai, kama vile marufuku au kufungwa kwa akaunti.
Huenda tutakuomba idhini yako ili kukusanya au kutumia Maelezo yako ya Kibinafsi kwa madhumuni maalum. Hii inajumuisha, kwa mfano, kutoa majarida, barua pepe za moja kwa moja, na hojaji kuhusu bidhaa na/au Huduma zetu na pia vipengele vingine fulani vya uuzaji.
Tunategemea nia kadhaa halali katika matumizi na kushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi. Nia hizi zinajumuisha: kukupa huduma ya mteja au usaidizi wa kiufundi ulioagiza, kuondoa hitilafu na kuimarisha Huduma zetu za sasa na za siku zijazo, ili kukupa maudhui ya kibinafsi, kubinafsisha huduma yako mtandaoni na kuwasiliana nawe kulingana na mapendeleo husika ya uuzaji, kuchunguza njia za kuboresha na kukuza operesheni zetu, kuhakikisha usalama wa Huduma zetu, na kwa uwekaji, utekelezaji au utetezi wa madai ya kisheria au wakati wowote mahakama zinatenda katika mamlaka zao za kimahakama.
Tunasindika Maelezo yako ya Kibinafsi ili kuambatana na jukumu letu la kisheria.
Unaweza kupinga usindikaji wa Maelezo yako ya Kibinafsi kulingana na nia halali kwa misingi inayohusiana na hali yako. Unaweza kudhibiti kiwango cha uuzaji tunaoelekeza kwako na una haki ya kutuomba kuacha kukutumia ujumbe wa uuzaji wakati wowote kwa kutumia maelezo ya mawasiliano yaliyoorodheshwa hapa chini.
Katika hali fulani, unaweza kuomba kwamba tuhamishe Maelezo ya Kibinafsi ambayo umetupatia. Unaweza kutuma ombi lako kwetu kama ilivyobainishwa katika sehemu ya Wasiliana Nasi hapa chini.
Wakati ambapo tunategemea idhini yako ili kusindika Maelezo yako ya Kibinafsi, una haki ya kuondoa idhini hiyo kwa matumizi zaidi ya Maelezo yako ya Kibinafsi wakati wowote.
Ikiwa wewe ni mgeni kwenye Tovuti au bidhaa na huduma nyingine za mtandaoni kutoka nje ya Marekani, Maelezo ya Kibinafsi unayotupatia yatakusanywa, kusindikwa na kuhifadhiwa moja kwa moja kwenye, au kuhamishwa hadi, seva zilizo nchini Marekani au nchi nyingine ambazo huenda zikawa hazina sheria sawia za ulindaji data kama nchi ambako unaishi.
Unapotuma Maelezo yako ya Kibinafsi nje ya EEA tunategemea ulinzi mwafaka au unaofaa unaopatikana chini ya sheria husika za ulindaji data. Kwa mfano, tunapotuma Maelezo ya kibinafsi yaliyokusanywa katika EU hadi maeneo nje ya EEA, tunategemea mbinu ya utumaji inayotumika na Tuma ya Ulaya (European Commission) ili kutusaidia kuhakikisha ulinzi tosha, kama vile Kauli za Kawaida za Kimkataba au idhini ya mtu binafsi ya kutuma Maelezo ya Kibinafsi kutoka EEA hadi nchi nje ya EEA. Kwa kutumia Huduma zetu, moja kwa moja unatoa idhini ya ukusanyaji, utumaji na usindikaji huo. Pia huenda tukahitaji kutuma Maelezo yako ya Kibinafsi ili kukupa Huduma kulingana na makubaliano yaliyopo baina yako na sisi.
Ikiwa unaishi EU, baada ya kutuma ombi, tutakupa maelezo kuhusu kana kwamba tuna Maelezo yako yoyote ya Kibinafsi pamoja na maelezo yoyote tunayohitajika kukupa chini ya sheria husika. Katika matukio fulani, pia huenda ukawa na haki ya:
Ili kutuma ombi, tafadhali wasiliana nasi kama ilivyobainishwa katika sehemu ya Wasiliana Nasi hapa chini. Tutajibu ombi lako kwa muda unaofaa.
Pia una haki ya kuondoa idhini yako ya kusindika Maelezo yako ya Kibinafsi, ikiwa uwezo wetu wa kusindika unategemea idhini yako pekee. Unaweza kufanya hivi kwa kuacha kutumia Huduma, ikiwa ni pamoja na kufunga akaunti zako zote za mtandaoni ulizosajili nasi na kuwasiliana nasi kama ilivyobainishwa katika sehemu ya Wasiliana Nasi hapa chini ili kuomba Maelezo yako ya Kibinafsi yafutwe. Ukiondoa idhini yako ya kutumia na kushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi kwa madhumuni yaliyobainishwa karika Sera hii ya Usiri, hautaweza kufikia Huduma zote (au yoyote), na huenda hatutaweza kukupa Huduma zote (au yoyote). Tafadhali kumbuka kwamba, katika matukio fulani, huenda tukaendelea kusindika Maelezo yako ya Kibinafsi baada ya wewe kuondoa idhini yako na kuomba tufute Maelezo yako ya Kibinafsi, ikiwa tuna msingi wa kisheria kufanya hivo. Kwa mfao, huenda tukasalia kuhifadhi maelezo fulani ikiwa tunahitajika kufanya hivyo ili kuambatana na jukumu huru la kisheria, au ikiwa ni muhimu kufanya hivyo ili kutimiza nia zetu halali katika kudumisha Huduma.
Ikiwa una malalamishi yoyote kuhusu mazoea yetu ya usiri, tunakuomba uwasiliane nasi kama ilivyobainishwa katika sehemu ya Wasiliana Nasi hapa chini. Pia una haki ya kuwasilisha lalamishi kwa mamlaka ya ulindaji data ya kitaifa (yaani, mamlaka simamizi).
Bull City Learning, Inc.
[email protected]