Sera ya Usiri

Bull City Learning, Inc.

Sera ya Usiri

Bull City Learning, Inc., ikijumuisha washirika wake ("Bull City Learning", "sisi", "yetu", au "zetu") wanajitahidi kudumisha ulinzi imara wa usiri wako, iwe ni wa kibinafsi au kwa niaba ya mhusika mwingine ("wewe" au "mtumiaji").  

Sera yetu ya Usiri ("Sera ya Usiri" au "Makubaliano" haya) imebuniwa ili kukusaidia uelewe jinsi tunavyokusanya, tunavyotumia na tunavyolinda maelezo unayotupatia au ili kukusaidia katika kufanya maamuzi kwa ufahamu unapotumia Huduma yetu.   Madhumuni ya Makubaliano haya, neno "Tovuti" linarejelea tovuti yetu, blogi zetu, akaunti zetu za mitandao ya kijamii, au programu zetu kwa ambazo huduma ya Bull City Learning inaweza kufikiwa ambapo watumiaji wanaweza kutazama tovuti na kujisajili kutumia programu, bidhaa, na/au huduma zetu (moja ni "Huduma," na kwa pamoja ni "Huduma").

Usiri wako ni muhimu kwetu. Kwa hivyo, tafadhali chukua muda wako kusoma Sera hii ya Usiri kwa makini. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu jinsi tunavyokusanya, tunavyotumia, tunavyolinda, au vinginevyo tunavyoshughulikia Maelezo yako ya Kibinafsi (kama ilivyoelezewa hapa chini), tafadhali wasiliana nasi.

Isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo katika Sera hii ya Usiri, maneno yaliyotumiwa katika Sera hii ya Usiri yana maana sawia na ilivyotumika katika Sheria za Huduma na yako chini ya sheria na masharti yaliyobainishwa hapa. Kwa kutumia Huduma, unatoa ridhaa ya sisi kukusanya, kuhifadhi, kutumia na kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi chini ya masharti yaliyobainishwa hapa.

I.               MAELEZO TUNAYOKUSANYA

Tunakusanya "Maelezo Yasiyo ya Kibinafsi" na "Maelezo ya Kibinafsi."  Maelezo Yasiyo ya Kibinafsi yanajumuisha maelezo ambayo hayawezi kutumika kukutambulisha kibinafsi, kama vile data za matumizi bila jina lako, maelezo jumla ya kidemografia tunayoweza kukusanya, kurasa na viungo vinavyoelekeza, aina ya majukwaa, mapendekezo unawasilisha, na mapendekezo ambayo kiujumla yana msingi kwenye data unazowasilisha na idadi ya mara unayobonyeza.  Maelezo ya Kibinafsi yanajumuisha barua pepe yako, nambari yako ya simu, anwani yako na maelezo mengine yoyote unayowasilisha kwetu kupitia Tovuti. Tunakusanya maelezo yanayokuhusu kwa madhumuni ya kuendesha Huduma. Maelezo haya yanajumuisha lakini sio tu jina lako, eneo lako, cheo chako kazini, anwani yako ya barua pepe, na maelezo mengine ya mawasiliano, metriki kuhusiana na mara unayotumia Huduma, na mapendeleo ya lugha.

1.   Maelezo yaliyokusanywa kupitia Teknolojia. Katika juhudi za kuimarisha ubora wa Huduma, tunafuatilia maelezo tunayopatiwa na kivinjari chako au na programu yetu unapotazama au unapotumia Huduma, kama vile unatoka kwa tovuti ipi (inajulikana na "Kiungo kinachoelekeza"), aina ya kivinjari unachotumia, kifaa unachotumia kuunganisha na Huduma, saa na tarehe unapofikia Huduma, na maelezo mengine ambayo hayakutambulishi kibinafsi.  Tunafuatalia maelezo haya kwa kutumia kuki, au faili ndogo za maandishi ambazo zinajumuisha vitambulishi vya kipekee bila jina.  Kuki zinatumwa kwenye kivinjari cha mtumiaji kutoka kwenye seva zetu na zinahifadhiwa kwenye hifadhi kuu ya kompyuta ya mtumiaji.  Kutuma kuki kwenye kivinjari cha mtumiaji kunatuwezesha kukusanya Maelezo Yasiyo ya Kibinafsi kumhusu mtumiaji na kuweka rekodi ya mapendeleo ya mtumiaji anapotumia Huduma zetu, kibinafsi na pia kama kadirio. Bull City Learning inaweza kutumia kuki za kudumu na pia za kila kipindi; kuki za kudumu zinasalia kwenye kompyuta yako baada ya kufunga kipindi chako na mpaka wakati utazifuta, ilhali kuki za kipindi zinafutwa unapofunga kivinjari chako.   

2.   Maelezo unayotupatia kwa kusajili akaunti. Kando na maelezo yanayopatianwa na kivinjari chako kiotomatiki unapotembelea Tovuti, ili kuwa mteja wa Huduma, utahitajika kutengeneza wasifu wa kibinafsi.  Unaweza kutengeneza wasifu kwa kujisajili kwenye Huduma na kuweka majina yako kamili, nambari yako ya simu, anwani yako ya barua pepe, na maelezo mengine ya kibinafsi na kutengeneza jina la mtumiaji pamoja na nenosiri.  Kwa kujisajili, unatuorodhesha kukusanya, kuhifadhi, na kutumia anwani yao ya barua pepe kulingana na Sera hii ya Usiri. 

II.             JINSI TUNAVYOTUMIA NA TUNAVYOSHIRIKI MAELEZO 

Maelezo ya Kibinafsi:

Isipokuwa iwe imetajwa vinginevyo katika Sera hii ya Usiri, hatuuzi, kufanyisha biashara, kukodisha, au vinginevyo kushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi na wahusika wengine kwa madhumuni ya uuzaji bila idhini yako. Tunashiriki Maelezo ya Kibinafsi na wachuuzi ambao wanawasilisha huduma kwa niaba ya Bull City Learning, kama vile utangamano na wahusika wengine.  Wachuuzi hao wanatumia Maelezo yako ya Kibinafsi tu chini ya uelekezi wetu na kulingana na Sera yetu ya Usiri. Kwa ujumla, Maelezo ya Kibinafsi unayotupatia yanatumiwa kutusaidia kuwasiliana nawe.  Kwa mfano, tunatumia Maelezo ya Kibinafsi kuwasiliana na watumiaji tunapojibu maswali, kuomba maoni kutoka kwa watumiaji, kutoa usaidizi wa kiufundi, na kuwaarifu watumiaji kuhusu ofa za promosheni.

Huenda tukakutumia ofa na maelezo yanayohusiana na Huduma zetu kwa mabzo unaweza kujiodoa kupitia kitufe cha kujiondoa (unsubscribe) kilicho katika barua pepe. Huenda tukakutumia maelezo muhimu kuhusiana na akaunti, ambayo hauwezi kujiondoa ili kutoyapokea tena. 

Maelezo Yasiyo ya Kibinafsi:

 Kwa ujumla, tunatumia Maelezo Yasiyo ya Kibinafsi ili kutusaidia kuimarisha Huduma na kubinafsisha huduma kwa mtumiaji.  Pia tunafanya makadirio ya Maelezo Yasiyo ya Kibinafsi ili kufuatilia mitindo na kuchambua mitindo ya matumizi kwenye Tovuti.  Sera hii ya Usiri kwa njia yoyote haiwekei vikwazo matumizi na ufichuaji Maelezo Yasiyo ya Kibinafsi na tunahifadhi haki ya kutumia na kufichua Maelezo hayo Yasiyo ya Kibinafsi kwa wabia wetu, watangazaji wetu na wahusika wengine kwa hiari yetu. Endapo tutapitia muamala wa kibiashara kama vile uunganishwaji, kununuliwa na kampuni nyingine, au kuuzwa kikamilifu au sehemu ya mali yetu, Maelezo yako ya Kibinafsi huenda ikawa mojawapo ya mali inayouzwa.  Unakiri na kutoa ridhaa kwamba ununuzi huo unaweza kufanyika na unaruhusiwa na Sera hii ya Usiri, na kwamba mnunuzi yeyote wa mali yetu anaweza kuendelea kusindika Maelezo yako ya Kibinafsi kama ilivyobainishwa katika Sera hii ya Usiri.  Mazoea yetu ya kusindika maelezo yakibadilika wakati wowote katika siku zijazo, tutachapisha mabadiliko ya sera kwenye Tovuti ili uwe na fursa ya kujiondoa kwenye mazoea hayo mapya ya kusindika maelezo.  Tunapendekeza kwamba ukague Tovuti mara kwa mara ikiwa una wasiwasi kuhusu jinsi maelezo yako yanavyotumiwa. 

III.          MAELEZO YANAYOTUMIKA BAINA YA WATUMIAJI; UTUMAJI UJUMBE BAINA YA WATUMIAJI

Matumizi yako ya Tovuti yanaweza kuhusu kusajili akaunti kwenye Tovuti na kutengeneza wasifu wa kibinafsi kwa ambao utapakia maelezo fulani ya kibinafsi, ikijumuisha picha yako ya wasifu, jina, eneo (nchi), cheo cha kitaalamu, lugha inayopendelewa, na shughuli za akaunti (ikijumuisha idadi ya video ulizotazama, video ulizotazama, muda uliotumia kutazama video, video ulizohifadhi kwenye orodha za utazamaji, video "ulizopenda", beji ulizopata, na video ulizoshiriki za wengine. Kimsingi, maelezo haya yanapatikana kuonwa na watumiaji wengine waliosajiliwa. Hata hivyo, una chaguo la kufanya baadhi ya maelezo haya kuwa ya siri/kibinafsi na hivyo basi hayataonwa na watumiaji wengine waliosajiliwa. Bado utaweza kutazama maelezo ya watumiaji wengine ambayo yanaweza kuonekana. Maelezo ya wasifu yanaweza kuonwa tu na watumiaji wengine ambao wameunda akaunti iliyosajiliwa; hayawezi kuonwa na watu wanaotembelea tovuti bila kusajili akaunti.

Matumizi yako ya Tovuti huenda yakahusisha Huduma zinazowezesha mawasiliano baina yako na watumiaji wengine kupitia jukwaa la ujumbe wa majadiliano au mbinu za mawasiliano za kielektroniki. Idadi ya ujumbe unaopokea, na kana kwamba unapokea ujumbe wowote au la, inatofautiana kulingana na Huduma unazotumia na kiwango cha utangamano wako na watumiaji wengine wa Tovuti.

Mawasiliano yote baina yako na watumiaji wengine yako chini ya Vikwazo vya Matumizi na Kanusho la Maudhui Mtandaoni, kama jinsi kila moja ilivyobainishwa kwenye Sheria za Huduma za tovuti yetu. Unakubali kutuondolea lawama kikamilifu kwa madai, gharama, na hasara zote zinazoibuka kutokana au kuhusiana na ukosefu wako wa kuambatana na sheria hizi. Ukiamua kushiriki maelezo ya kibinafsi na watumiaji wengine kupitia mawasiliano baina yako na wao kwenye Tovuti, unafanya hivyo kwa shauri yako, kwani hatuwezi kutoa hakikisho kwamba usiri wa maelezo hayo ya kibinafsi utalindwa. Aidha, ikiwa mawasiliano baina yako na watumiaji wengine kwenye Tovuti yatapelekea, mbinu nyingine za mawasiliano za nje ambazo hazihusiani na Tovuti, unawakilisha na kukiri kwamba mawasiliano hayo hayako chini ya ulinzi wa Sheria za Huduma wala Sera hii ya Usiri. Unajihusisha katika mawasiliano hayo kwa shauri yako.

IV.             JINSI TUNAVYOLINDA MAELEZO

Tunatekeleza hatua za kiusalama zilizobuniwa kulinda maelezo yako dhidi ya kufikiwa bila idhini.  Akaunti yako inalindwa na nenosiri la akaunti yako na tunakusihi uchukue hatua ili kuweka maelezo yako ya kibinafsi salama kwa kutofichua nenosiri lako na kwa kutoka (log out) kwenye akaunti yako baada ya kila matumizi.  Aidha tunalinda maelezo yako dhidi ya ukiukaji wa kiusalama unaoweza kutokea kwa kutekeleza hatua fulani za kiusalama za kiteknolojia ikijumuisha, usimbaji, kuta za usalama na teknolojia ya ukuta wa soketi ya usalama.  Hata hivyo, hatua hizi hazihakikishii kwamba maelezo yako hayatafikiwa, kufichuliwa, kubadilishwa, au kuharibiwa baada ya hatua hizo za usalama na programu ya seva salama kukiukwa.  kwa kutumia Huduma zetu, unakiri kwamba unaelewa na unakubali kuchukua hatari zote. 

V.           HAKI ZAKO KUHUSIANA NA MATUMIZI YA MAELEZO YAKO YA KIBINAFSI

Wakati wowote una haki ya kutuzuia kuwasiliana nawe kwa madhumuni ya uuzaji.  Tunapotuma mawasiliano ya promosheni kwa mtumiaji, mtumiaji huyo anaweza kujiondoa kutopokea mawasiliano zaidi ya promosheni kwa kufuata maagizo ya kujiondoa yaliyo kwenye kila barua pepe ya promosheni. Tafadhali kumbuka kwamba bila kujali mapendeleo ya mawasiliano ya promosheni unayobainisha kwa kujiondoa katika sehemu ya Mipangilio ya Tovuti, huenda tukaendelea kukutumia barua pepe za kiutawala, kwa mfano, masasisho ya mara kwa mara kwenye Sera yetu ya Usiri, au maelezo mengine muhimu ya akaunti. 

VI.             DATA ZA MTEJA 

"Data za Mteja" inamaanisha maelezo yote yanayosindikwa au kuhifadhiwa kwenye Huduma na Mteja au kwa niaba ya Mteja, na pia maelezo yoyote yanayotokana na maelezo hayo. Data za Mteja zinajumuisha, lakini sio tu: (1) maelezo yaliyotolewa kwenye Huduma;(2) maelezo yaliyopatiwa Bull City Learning na watumiaji wengine au na wahusika wengine; na (3) maelezo yanayoweza kumtambulisha mhusika kibinafsi kutoka kwa wateja, watumiaji, au wahusika wengine. 

(a)  Ufikiaji, Matumizi, na Amri za Kisheria. Isipokuwa ipokee idhini ya awali ya Mteja kwa maandishi, Bull City Learning:

  • haitafikia, kusindika, au vinginevyo kutumia Data za Mteja isipokuwa kama inavyohitajika ili kuwezesha Huduma;
  • haitapea waajiriwa wake wowote ufikiaji wa Data za Mteja isipokuwa kwa kiwango ambacho mtu huyo anahitaji ili kuwezesha utendakazi wake chini ya Makubaliano haya na matumizi hayo yako chini ya makubaliano mwafaka ya kutofichua waliyokubaliana na Bull City Learning yanayolinda data hizo, masharti yake yakiwa sawia na yale yaliyo kwenye Sehemu hii; na
  • haitampa mhusika mwingine yeyote ufikiaji wa Data za Mteja. Bila kujali yaliyotajwa hapa juu, Bull City Learning inaweza ikafichua Data za Mteja kama inavyohitajika na sheria husika au na mamlaka mwafaka ya kisheria au kiserikali. Bull City Learning itampa Mteja ilani bila kuchelewa kuhusu amri yoyote kama hiyo ya kisheria au kiserikali na kushirikiana na Mteja katika juhudi za kutafuta amri ya kujilinda au vinginevyo kupinga ufichuaji huo, kwa gharama ya Mteja. 


(b)  Haki za Mteja. Isipokuwa iwe imetajwa katika Makubaliano haya, Mteja na haki na anahifadhi haki zote kuhusiana na Data za Mteja, na matumizi au uhifadhi wa Bull City Learning wa data hizo ni kwa niaba ya Mteja pekee.

VII.             VIUNGO KUELEKEA TOVUTI NYINGINE

Kama sehemu ya Huduma, tunaweza kutoa viunganisho kwa tovuti au programu nyingine.  Hata hivyo, hatuwajibikii mazoea yausiri yanayotumiwa na tovuti hizo au maelezo au maudhui yaliyo kwenye tovuti hizo.  Sera hii ya Usiri inatumika tu kwa maelezo yaliyokusanywa kupitia Tovuti na Huduma.  Hivyo basi, Sera hii ya Usiri haitumiki kwa matumizi ya tovuti ya wahusika wengine inayofikiwa kwa kuchagua kiungo kwenye Tovuti yetu au kupitia Huduma zetu.  Kwa kiwango unachofikia au kutumia Huduma kupitia au kwenye tovuti au programu nyingine, basi sera ya usiri ya tovuti au progtamu hiyo nyingine itatumika kwenye ufikiaji wako au matumizi yako ya tovuti au programu hiyo.  Tunawahamasisha watumiaji wetu wasome kauli za usiri za tovuti nyingine kabla ya kuendelea kuzitumia. 

VIII.           MABADILIKO KWENYE SERA YA USIRI

Bull City Learning inahifadhi haki ya kubadilisha sera hii na Sheria zetu za Matumizi wakati wowote.  Tutakuarifu kuhusu mabadiliko makubwa kwenye Sera yetu ya Usiri kwa kutuma ilani kwa anawani msingi za barua pepe zilizobainishwa kwenye akaunti yako au kwa kuweka ilani kwenye tovuti yetu.  Mabadiliko makubwa yataanza kutumika siku 30 kufuatia ilani hiyo arifa hiyo kutolewa.  Mabadiliko ambayo si makubwa yataanza kutumika maramoja. Unapaswa kukagua Tovuti mara kwa mara na pia ukurasa huu wa usiri ili kupata masasisho. 

IX.       HAKI ZA USIRI JIMBONI CALIFORNIA

Ikiwa wewe ni mkaazi wa California, huenda ukawa na haki za ziada za usiri. Ili kupata maelezo kamili kuhusu haki hizo, tafadhali tazama Haki na Ufichuaji wa California.

X.             WATEJA AU WATUMIAJI NJE YA MAREKANI

Ikiwa wewe ni mkaazi wa mamlaka iliyo nje ya Marekani, tafadhali tazama Ufichuaji katika Eneo la Kiuchumi la Ulaya na wa Mamlaka nyingine Nje ya Marekani.

XI.             WASILIANA NASI

Ikiwa una maswali yoyote kuhusiana na Sera hii ya Usiri au mazoea ya Tovuti hii, tafadhali wasiliana nasi kwa kutuma barua pepe kwa anwani [email protected].

Sera hii ya Usiri ilisasishwa mwisho mnamo Machi 23, 2020.