IA Watch Yaanzisha Vipengele vya Kijamii kwa ajili ya Jumuiya

Unganishwa na wataalamu wa chanjo duniani kote.

Ingia Mtumiaji Mpya? Jiandikishe sasa

Tumeongeza upatikanaji mkubwa wa IA Watch: Jamii yetu ya maelfu ya wataalamu wa chanjo. Sasa, unaweza kuuliza maswali, kuunganishwa na wenzako kupitia orodha ya wanachama, na kuona jinsi wengine wanavyosonga mbele na ufahamu wao wa chanjo kupitia orodha ya wanaoongoza na orodha ya kutazama ionekanayo kwa wote.

Hivi ndivyo unavyoweza kutumia vipengele vipya vya kijamii kwenye IA Watch ili kushirikiana na watumiaji wengine waliojisajili.

Tafuta Wanachama Wengine

Unaweza kuangalia wasifu mmoja mmoja katika orodha ya wanachama, ambayo inasaidia kuwatafuta na kuunganishwa na wenzako. Unaweza kuperuzi wasifu za wanachama, kuzipangilia kwa majina au nchi, au kutafuta wenzako walio katika kazi maalum, kwa kutumia chujio.

IA Watch Member Directory
Sambaza Orodha ya Kutazama

Unaweza kuona orodha za video zilizotazamwa na wanachama wengine ambazo wamezitengeneza kwa ajili ya kujielimisha wenyewe, na video walizotazama, walizozipenda au walizosambazia wengine. Tafuta watumiaji wanaopenda vitu vinavyofanana na vyako au jifunze kupitia orodha za utazamaji wa video walizotengeneza.

IA Watch watchlist
Ona Wanachopendekeza Wataalamu

Tumeshirikiana na wataalamu wa chanjo ili kukupa orodha za utazamaji zilizoandaliwa vizuri, ambazo zinaweza kuitwa katika sehemu mbalimbali za tovuti. Kila orodha ya utazamaji ya mtaalamu itaonyesha video mbalimbali ambazo mtaalam huyo anayeheshimika duniani anaona ni sahihi na zinafaa. Utaweza kujifunza zaidi kuhusu wataalamu kwa kuangalia wasifu zao.

IA Watch expert watchlist
Jishindie njia ya kuingia katika orodha ya wanaoongoza

Ili kuonyesha maendeleo ya wanachama wetu wanaojituma zaidi, tunaanzisha orodha ya wanaoongoza kwenye kurasa za mada. Orodha ya wanaoongoza itaonyesha msimamo wa wanafunzi bora katika kila mada, ukipangwa kwa kufuata mafanikio yao. Ongeza hadhi yako kwenye kila kipengele kwa kutazama video, ambayo itakusaidia kukupatia nafasi kwenye orodha ya wanaoongoza kati ya wenzako waliofanikiwa sana.

IA Watch leaderboard
Tuma Ujumbe kwa Wenzako

Jiunge na jamii ya IA Watch kupitia kipengele kipya cha kutuma ujumbe. Uliza maswali sahihi na sambaza majibu kwenye kurasa za jumbe za mada, ambazo zinaatikana na watumiaji wote waliosajiliwa.

IA Watch message board
Tumia Dakika Chache Kukamilisha Wasifu Wako

Ikiwa tayari una akaunti, tunakusihi ukamilisha wasifu wako kwa kuweka picha, kazi na nchi yako. Ikiwa haujawahi kusajili akaunti, sajili sasa ili uanze kuitumia. Wasifu wote wa IA Watch utaonekana na watumiaji wengine waliojisajili. Ikiwa utapenda kuwa na wasifu binafsi, au kuzuia kile ambacho watumiaji wengine wanaweza kuona, unaweza kupata mipangilio yako ya faragha kupitia ukurasa wako wa wasifu.

IA Watch Profile Edit

Unda akaunti yako leo ili kupata vipengele vipya vya IA Watch na jiunge na kundi letu la wataalam wa chanjo duniani.

Jiandikishe sasa